Mwanamke mmoja mfanyibiashara nchini Mexico ambaye alikuwa akiliongoza kundi moja la familia 600 linalowatafuta ndugu zao waliopotea ameuawa.
Miriam Rodriguez Martinez alipigwa risasi nyumbani kwake katika mji wa San Fernando katika jimbo la Tamaulipas.
Alijipatia umaarufu mkubwa kwa kufanikiwa kuchunguza utekaji na mauaji ya mwanawe yaliotekelezwa na kundi moja la ulanguzi wa mihadarati , The Zetas.
Habari aliyotoa kwa maafisa wa polisi ilihakikisha kuwa wanachama wa kundi hilo wanafungwa jela.
Lakini mnamo mwezi Machi, mmoja wao alitoroka na wenzake wanasema alianza kupokea vitisho.
Aliuawa siku ya akina mama nchini Mexico 10 mwezi Mei.
Wenzake wanasema kuwa alikuwa ameomba ulinzi kutoka kwa polisi lakini akapuuziliwa mbali.
Mwendesha mashtaka Irving Barrios aliambia mkutano wa wanahabari kwamba usalama ulikuwa umeimarishwa na kwamba maafisa wa polisi walikuwa wakipiga doria mara tatu kwa siku.
Hatahivyo familia yake imekana hilo.
Shirika la kulinda haki za kibinaadamu nchini Mexico lilituma ujumbe wa Twitter likishutumu mauaji hayo.
Maandamo ya kupinga kupotea kwa watu nchini Mexico
Bi Rodriguez ni mwanzilishi wa kund hilo la familia ambalo limekuwa likiathiriwa na ghasia tangu mwanawe Karen Alejandro kutekwa 2012.
Alifanikiwa kuupata mwili wa mwanawe katika kaburi la kisiri na kuwafunga wauaji wake jela.
Pia alitibua jaribio la utekaji lililotekelezwa na Zetas la mumewe wakati alipolifukuza genge hilo kwa kutumia gari lake na kuliarifu jeshi ambalo liliwakamata watekaji hao .
Kulingana na mmoja ya wanaharakati wenzake Bi Rodruiguez alihisi hawezi kusubiri tena baada ya wauaji wa mwanaye kukamatwa.
Kundi hilo la familia lilianza baada ya kupotea kwa watoto 43 mnamo mwezi Oktoba 2014 kutoka Ayotzinapa kusini magharibi mwa jimbo la Guerrero.
0 Post a Comment:
Post a Comment