Polisi nchini Cambodia imewakamata watu wawili wakishutumiwa kuwasafirisha watu takriban kumi kwenda nchini India kwa ajili ya kuchangia figo zao kwa ajili ya shughuli haramu ya kupandikiza viungo.
Watu hao, Mwanaume na mwanamke wanaoishi katika mji wa Phnom Penh wanaelezwa waliandaa safari hiyo kwa watu hao kwa ahadi ya malipo ya dola za kimarekani 6000 kila mmoja.
Raia wa Cambodia wenye uhitaji wa figo waliwalipa watu hao wawili dola 40,000 za Marekani kwa ajili ya Operesheni hiyo ya kupandikiza figo, nchini India.
Mwaka jana,Serikali ya Cambodia ilipiga marufuku biashara ya viungo, inayodaiwa kuwa haramu.
0 Post a Comment:
Post a Comment