Mgombea aliyekuwa awanie uchaguzi mkuu wa Iran utakaofanyika siku ya Ijumaa amejiondoa ili kumsaidia Rais wa nchi hiyo Hassan Rouhani kushinda kwa mara ya pili.
Eshaq Jahangiri ambaye ni makamu wa Rais nchini humo, amewaambia wafuasi wake kuwa atapiga kura yake kwa Rais aliyepo madarakani hivi sasa.
Ebrahim Raisi (kushoto)
Jumatatu Meya wa jiji la Tehran Mohammed Baqr Qalibaf alijiondoa katika mbio hizo na kumuunga mkono Ebrahim Raisi anayegombea upande wa upinzani.
Kujiondoa kwa wagombea hao kumafanya kazi kuwa nyepesi zaidi kwa Rais aliyepo madarakani Hassan Rouhani ambaye atachauana na Ebrahim Raisi.
0 Post a Comment:
Post a Comment