Muungano wa wanjeshi dhidi ya kundi la Islamic State unaendelea kukabiliana na kundi hilo nchini Syria
Waziri wa nchi za kigeni nchini Uturuki, Mevlut Cavusoglu ameiambia Marekani imhamishe balozi wake nchini Syria kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Kikurdi nchini humo, (YPG).
Bw Mevlut amesema ni wazi kuwa balozi wa marekani kwa muungano dhidi ya IS, Brett McGurk, anayaunga mkono makundi ya YPG na PKK
Wapiganaji wa YPG wanakabiliana na kundi la Islamic State lakini Uturuki inaona YPG kuwa kundi la kigaidi.
Waziri Mevlut alizungumza nchini Marekani akiandamana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye alifanya kikao na rais Donald Trump.
Baada ya kurejea mjini Ankara, waziri huyo ameviambia vyombo vya habari kuwa wamehakikishiwa mji wa Raqqa, utarudishiwa wenyeji wa kiarabu baada ya oparesheni ya kuwaondoa IS unaondelea kukamilika.
Aidha, Rais Erdogan amepiga jeki kauli ya waziri wake akiongeza kuwa Uturuki itashambulia bila kumuuliza yeyote iwapo litashuhudia uvamizi kutoka kundi la Kikurdi nchini Syria.
Mbali na hayo mvutano kati ya Uturuki na Marekani umeendelea baada ya Uturuki kuwazuia wabunge 250 kuingia nchini humo.
Serikali ya Ujerumani imetishia kuwaondoa wanajeshi wake walioko kambi ya Incirlik nchini humo kutokana na hatua ya Uturuki.
Waziri Mevlut amesema Ujerumani inaweza kuwaondoa wanajeshi wake kwani ndio ilisaka ruhusa ya kuweka kambi eneo hilo.
Majibizano hayo yamelaumiwa kutokana na hatua ya Ujerumani kuwapa hifadhi wanajeshi walioshirki kwenye jaribio la kupindua serikali.
0 Post a Comment:
Post a Comment