Korea Kaskazini: Tulifanyia majaribio makombora ya kushambulia meli


9 Juni 2017

Korea Kaskazini ilionesha makombora ya kushambulia meli aina ya Styx katika maonesho ya kijeshi ya 2012
Korea Kaskazini ilionesha makombora ya kushambulia meli aina ya Styx katika maonesho ya kijeshi ya 2012

Korea Kaskazini imesema kuwa makombora iliyoyafanyia majaribio siku ya Alhamisi yalikuwa ni aina nyingine ya makombora ya maroketi ya ardhini na baharini.
Makombora hayo yameundwa mahsusi kushambulia "kundi la meli za kivita" ambazo zimekuwa zikiitishia Korea Kaskazini.
Majaribio hayo ya jana yalikuwa ya hivi karibuni katika msururu wa vitendo vya ukiukaji wa vikwazo vya Umoja wa mataifa na yalishuhudiwa na kiongozi wan chi hiyo Kim Jong-Un, shirika la habari la serikali la Korean Central News Agency limesema.
Majaribio hayo yamefanyika siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kuongeza makali ya vikwazo dhidi ya taifa hilo.
"Makombora hayo yaliyorushwa yaliweza kutambua kwa ufasaha vifaa vilivyolengwa vilivyokuwa vinaelea kwenye bahari ya mashariki mwa Korea," KCNA walisema, wakizungumzia Bahari ya Japan, ambako kuna meli mbili kubwa za Marekani za kubeba ndege za kivita.
Meli hizo za USS Carl Vinson na USS Ronald Reagan ziliongoza mazoezi ya siku tatu ambayo yalimalizika Juni 3 yakihusisha meli zaidi ya kumi za kivita za Marekani pamoja na mbili za Japan.
Mazoezi hayo yalionekana kulenga kuitisha Korea Kaskazini.
Marekani imezidisha shughuli zake zakuonesha ubabe wa kijeshi eneo hilo, ambapo ina nyambizi inayotumia nguvu za nyuklia, USS Cheyenne yenye uzani wa tani 6,900, ambayo kawaida huwa Pearl Harbor.
Manowari hiyo iliwasili katika bandari ya Busan nchini Korea Kusini Jumanne.
Gazeti kuu la Korea Kaskazini Rodong Sinmun lilichapisha picha za Kim akitabasamu akiwa amezingirwa na majenerali kadha waliovalia sare za kijeshi kwenye ukurasa wake wa kwanza.
Ndani, kulikuwa na picha zilizodaiwa kuonesha makombora yakirushwa kutoka kwa gari la kivita lililofanana na kifaru, na makombora hayo yakaonekana kufikia meli baharini.
Korea Kaskazini imefanya majaribio manne ya makombora tangu Rais wa sasa wa Korea Kusini Moon Jae-in alipochukua madaraka Mei.
Haki miliki ya pich
Makombora hayo ya Alhamisi yalipaa takriban kilomita 200, jambo ambalo linaonesha huenda taifa hilo limepiga hatua ukilinganisha na kombora la 2015 ambalo lilipaa kilomita 100 pekee.
KCNA walisema makombora hayo yaliyofanyiwa majaribio Alhamisi yalikuwa kwenye maonesho ya kijeshi yaliyoandaliwa Aprili 15 wakati wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa nchi hiyo Kim Il-Sung.
Silaha zote mpya ambazo zimekuwa katika maonesho hayo zimefanyiwa majaribio katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, isipokuwa moja ambalo lilionekana kuwa kama kombora la masafa marefu la kuweza kuruka kutoka bara moja hadi nyingine, shirika la habari la Yonhap liliripoti.


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: