Ureno kuomboleza vifo vya raia wake kwa siku tatu



19 Juni 2017

Ureno
Moto mkubwa ukiwaka wilayani Pedrogao Grande
Mamia ya wafanyakazi kutoka katika kikosi cha kupambana na majanga ya moto wanapambana ili kuudhibiti moto mkubwa uliozuka katika msitu mkubwa katikati mwa Ureno, ambao umeua watu sitini mpaka sasa.
Inaarifiwa kuwa watu wengi walifia katika gari zao wakati walipokuwa katika harakati za kuondoka katika eneo la tukio wilayani Pedrógão Grande. Akizungumza baada ya kutembelea eneo la tukio, waziri mkuu nchini humo , Antonio Costa, amesema kwamba wazima moto wamekwisha dhibiti mioto zaidi ya miamoja na hamsini nchini mwake.
Waziri Antonio ametangaza siku tatu za maombolezo na kueleza kuwa ni janga kubwa kwa nchi yake, kutoakana na kukabiliwa na majanga ya mioto mikubwa inayozuka katika misitu mikubwa miaka ya karibuni .
Vikosi viwili vya jeshi vimepelekwa katika eneo la tukio ili kuongeza nguvu na kutoa msaada wa dharula.
Umoja wa Ulaya,Ufaransa na Hispania kwa pamoja wamejitolea kutoa msaada wowote utakao hitajika, ikiwemo ndege za kupambana na mioto mikubwa kama hiyo.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: