Raila Odinga,Lowassa wamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta



 2 Juni 2017


Mgombea urais kupitia Muungano wa Vyama vya
Mgombea urais kupitia Muungano wa Vyama vya Upinzani (Nasa), Raila Odinga


Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa


 Wakati kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Kenya zikipamba moto, mgombea urais kupitia Muungano wa Vyama vya Upinzani (Nasa), Raila Odinga amesema Rais John Magufuli na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ni marafiki zake na hataki kumpoteza yeyote kati yao.
Odinga pia amesema anataka wawili hao kumuunga mkono katika harakati zake za kuwania urais.
Kauli ya mwanasiasa huyo mkongwe imekuja baada ya Lowassa kueleza wazi kuwa anamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta katika kampeni zake za kubakia Ikulu ya Kenya.
Lowassa, ambaye mwaka 2015 aligombea urais kwa tiketi ya Chadema na kuungwa mkono na vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa ameamua kumuunga mkono Kenyatta kwa sababu kwa kipindi alichokaa madarakani ameonyesha uwezo na amefanya kazi nzuri.
Baadaye Chadema ilitoa msimamo kuwa imeamua kumuunga mkono Kenyatta kwa kuwa Odinga anamuunga mkono Magufuli, ambaye ni rafiki yake.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema chama hicho kimefanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwa mtu pekee anayepaswa kuungwa mkono ni Kenyata kwani ndiye chaguo sahihi kwa wapenda demokrasia.
Alisema kuwa tangu zamani rafiki yao alikuwa ni Odinga na walimuunga mkono kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2012 lakini wakashangaa ilipofika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, mwaka 2015 Odinga akamuunga mkono Magufuli, aliyegombea urais kwa tiketi ya CCM.
Alimwagia sifa Uhuru Kenyata kuwa katika kipindi cha uongozi wake nchi hiyo ilitoa nafasi pana kwa vyama vya upinzani na akakuza demokrasia wala hakuna mpinzani aliyewekwa lumande kama Tanzania.
Lakini msemaji wa umoja huo wa wapinzani wa Kenya alitofautiana na hoja hizo.
“Odinga ni rafiki wa wote, JPM na Waziri Mkuu Lowassa,” unasema ujumbe mfupi wa simu alioutuma mkurugenzi wa mawasiliano wa ODM, Philip Etale.
“(Odinga) Aliweka bayana wakati wa kampeni za uchaguzi kuwa anawaunga mkono wote na kutaka mgombea bora ashinde. Kama ODM tunaamini katika demokrasia na tusingependa, wakati wowote ule, tupoteze marafiki zetu kwa sababu ya siasa.
“Odinga anataka kuungwa mkono na kila mtu na ni matumaini yetu kuwa uamuzi huo hautokana na uchaguzi uliopita bali mambo mengine.”
Uchaguzi wa Rais nchini Kenya utafanyika Agosti 8 na Kenyatta, mtoto wa muasisi wa taifa hilo, Jomo Kenyatta, anawania kuongoza Kenya kwa kipindi cha pili mfululizo.     
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: