Ajenti wa Korea Kaskazini akamatwa Australia

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Mwanamume mmoja amekatwa kwa madai kuwa alikuwa ajenti wa biashara wa Korea Kaskazini, kwa mujibu wa polisi nchini Australia.
Chan Han Choi, 59, ameshtakiwa kwa kuwa dalali kwa mauzo yaliyo kinyume na sheria kutoka nchini humo na kuzungumzia biashara ya silaha za maangamizi makubwa.
Polisi wanasema kuwa amevunja vikwazo wa Umoja wa Mataifa na Australia.
Kesi dhidi ya Bw Chan ambaye ameishi Australia kwa zaidi ya miaka 30 ni ya kwanza ya aina hiyo nchini humo.
Ndiyo mara ya kwanza mtu yeyote amestakiwa chani ya sheria za mwaka 1995 za silaha za nchi hiyo za maangimizi makubwa.
Polisi wanasema kuwa kuna ushahidi kuwa Bw. Chan, amekuwa akiwasiliania na maafisa wa vyeo vya juu wa Korea Kaskazini.
Wanadai kuwa alihusika na kutoa huduma za kuuza mipango ya silaha ya Korea Kaskazini ikiwemo kuuza teknolojia ya makombora ya masafa marefu kwa mataifa ya kigeni, ili kuutafutia fedha utawala wa Korea Kaskazini.
Bw Chan pia ameshtakiwa kwa kuhusika na uuzaji wa mkaa wa mawe kutoka Korea Kaskazini kwenda nchini Indonesia na Vietnam.
Anakabiliwa na mashtaka 6 kwa jumla baada ya kukamatwa nyumbani kwake siku ya Jumamosi usiku.
•Tuma habari picha na video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: