MADHARA YA SUMU KIROHO

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
17.12.2017 Jumapili
Somo: Madhara ya sumu kiroho
________________________________
By Askofu Nathan Meshack
#fgbfmwanza
Mwandishi: Zachary John Bequeker Mwanza 0625966236
_________________________________________________________
Askofu wa Jimbo la Iringa Nathan Meshack

Yakobo 3:1-12 ulimi hutoa sumu.Mafundisho tunayoyasikia mengine ni sumu ambayo hutulegeza na hata kutuua kiroho.
=> Wote tunataka kwenda mbinguni lakini kuna taratibu za kufanya ili kuingia mbinguni, huwezi kujiua ili uingie mbinguni Bali hadi Mungu mwenyewe aamue.
=> Hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kuua au kujiua, bali tumeruhusiwa kuua wanyama tu. Mungu ameturuhusu tule matunda Mwanza 2:16. Mungu ametupa ruhusa ya kula mboga za majani Mwanzo 3:18. Tuna ruhusa ya kula aina zote za wanyama Matendo 10:9-16.
=> Usiue ni moja ya amri kuu za Mungu Luka 18:18-20.
=> Hakuna sadaka ya kutoa uhai wa mtu.
=> Hata kutoa mimba ni kuua.
=> Kujinyonga au kunywa sumu ni kutafuta mauti ya milele.
=> Kuna watu wanao wapa sumu wengine ili wafe, hao wafanya dhambi.
_> Kama ambavyo hairuhusiwi kujiua au kuwaua watu wengine,vilevile hakuna ruhusa ya kuua au kujiua kiroho.
=> Kuna vyakula vya kiroho vingine vona sumu ambavyo hula watu na kuwafanya waishiwe nguvu za kiroho.
=> Siyo kila chakula tunachokula ni sahihi ni lazima tuwe makini juu ya mafundisho au mahubiri tunayoyasikia.
=> Vyakula vingine vya kiroho ni matango mwitu yanayoua 2 Falme 4:38-41.
=> Watu walioishiwa na nguvu za Mungu kwa nje huonekana wanaendelea na imani  hali wameshakufa kiroho Ufunuo 3:1-3.
NB: Kama uko katika sehemu venue mafundisho manyonge, chomoka sasa.1 Kor 2:15; Galatia 5:7-12. Na kama wewe ni mhubiri unafundisha na kuwalisha watu sumu badilika sasa, Kwanini kuwapa watu sumu Habakuki 2:15.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: