Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, amesema atampa malipo mazuri ya kustaafu Rais aliyeng`olewa mamlakani Robert Mugabe na mkewe.
Amesema kuwa Mugabe ataendelea kupokea mshahara wake na mafao mengine kama kawaida ikiwemo kusafiri katika kiwango cha kwanza kwenye ndege (first class), pamoja na kusafiri kwa gharama ya serikali.
Lakini Rais Mnangagwa amesema kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na asiyeweza kushtakiwa.
Na Amesema kuwa Zimbabwe itajiunga tena hivi kariubuni na mataifa ya jumuia ya madola.
'Hatujampa kinga mtu yoyote isipokua ambacho nimeahidi kwa rais aliyetangulia na baba wa taifa letu, rais Robert Mugabe ni kwamba tunampatia mafao na mshahara wake kama alivyokua akipata awali, usafiri, ofisi, ulinzi, na serikali yangu itamuwezesha kuenda Singapore kwenye matibabu, na vyote hivi mke wake pia ataviapata''.
Mnangagwa amesema pia serikali yake mpya inafanya jitahada kubwa za kupambana na rushwa.
'' Msimamo wangu ni kwamba Rushwa haiwezi kuvumiliwa hata kidogo, hatuwezi kabisa kuvumilia jambo kama hili , na kama mnafatilia mambo yanayotokea Zimbabwe kwa sasa , watu wengi wenye wadhifa mkubwa wamefikishwa mbele ya mahakama, na ni ndani ya miezi miwili tuu tayari tunawashughulikia watu wenye makossa ya rushwa''.
www.zakachekainjili.blogspot.com
+255625966236 Zachary John Bequeker
0 Post a Comment:
Post a Comment