Mama Salma Kikwete aapishwa rasmi katika bunge la Tanzania



Mama Salma Kikwete aapishwa rasmi katika bunge la Tanzania

  •  
Haki miliki ya picha                                                                                                                                                                                                
Image captionSalma Kikwete mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai leo amemuapisha mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Salma Rashid Kikwete kuwa mbunge wa Bunge wa kuteuliwa.
Mh.Salma aliandamana na mumewe rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, ambaye uwepo wake ulisababisha kelele za shamra shamra kutoka kwa wabunge wakisema kwa sauti 'tumekumiss tumekumiss'.
tweetHaki miliki ya pichaTWEETER
Mkutano wa saba wa bunge la Tanzania umeanza kikao chake cha kwanza cha mkutano wa bajeti hii leo.
Mama Salma kama anavyotambulika na wengi nchini ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, lakini pia anatajwa kuwa na ushawihi mkubwa sana wa kisiasa ndani ya chama chake.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: