Watoto wafariki dunia kwa madai ya kula ugali wenye sumu


Watoto wafariki dunia kwa madai ya kula ugali wenye sumu

 
By Anthony Mayunga,Mwananchi amayunga@mwananchipapers.co.tz
Serengeti. Watoto wawili wa familia moja wakazi wa Kijiji cha Gantamome wilayani Serengeti wamefariki baada ya kula ugali wa muhogo unaodaiwa kuwa na sumu.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 asubuhi baada ya familia hiyo kula ugali huo.
Waliokufa ni Mwikwabe Tugunye (14) na Mkami Tuguye (3), huku mama yao Nyabisi Tugunye (25) akinusurika.
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Selestin Mahiti alisema Aprili 2 mama wa watoto hao, aling’oa mihogo na kuiweka kwenye mifuko na Aprili 3 aliisaga na kupika ugali.
“Alfajiri ya Aprili 5 walianza kuumwa tumbo, kutapika na kuharisha na walikwenda zahanati iliyopo umbali wa kilomita tatu na kabla hawajaifikia mtoto mmoja alipoteza maisha,” amesema Mahiti.

  
 
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: