Upinzani Kenya wapanga kuhesabu kura uchaguzi ujao.



Vijana wanajisajili kupiga kura Kenya
Hisia tofuati zimeibuka nchini Kenya kufuatia kauli iliyotolewa hivi karibuni na upinzani National Supper Alliance (NASA) kuhusu mpango wa kuwa na kituo cha kuhesabia kura wakati wa uchaguzi mkuu Agosti, kitakacho endesha shughuli sambamba na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Vyombo vya habari Kenya, vinaripoti kuwa tume ya IEBC inasema mipango hiyo ya NASA itakwenda kinyume na sheria nchini.
Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga amekuwa akisisitiza tuhuma kwamba uchaguzi wa mwisho mnamo 2013, ulikumbwa na udanganyifu.
(IEBC) Mwenyekiti Wafula Chebukati
Image captionMwenyekiti wa (IEBC) Wafula Chebukati
Katika mkutano wa kisiasa hivi karibuni, bwana Odinga alinukuliwa na vyombo vya habari nchini akisema, 'Tunachotaka ni kuwa, katika kila kituo cha kuhesabu kura tutakuwa na vijana 50, watawasiliana na sisi kupitia video na kutujuza ni nani aliyepiga kura na ni nani ambaye hakupiga".

Ina maana gani kisheria?

Mratibu wa kitaifa kutoka jukwaa la uangalizi wa uchaguzi ELOG Mulle Musau anasema, ni kinyume cha sheria kuidhinisha vituo vya kupiga, kuhesabu na kutangaza kura wakati wa uchaguzi, kando na vituo rasmi vya tume ya uchaguzi nchini IEBC.
Kwa upande wa upinzani, inaweza kuruhusiwa kuwa na vituo maalum vinavyostahili kuwa vya kuendesha shughuli za chama hicho, wakati wa uchaguzi mkuu.
Musau anaongeza kuwa ili mradi chama hicho kitatumia matokeo ya mwisho yatakayo kuwa yanamiminika katika vituo mbali mbali vya tume rasmi ya uchaguzi Kenya IEBC, basi hakuna makosa.
Wafuasi wa ODM baada ya mahakama mnamo 2013 kuidhinisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta
Image captionWafuasi wa Raila baada ya mahakama Kenya mnamo 2013 kuidhinisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta
'Ni desturi ya vyama vya kisiasa nchini kufanya hivyo na ni jambo ambalo limekuwa likifanyika hata kwa waangalizi wa uchaguzi na vyombo vya habari katika kufuatilia matokeo'.
Hofu iliopo ni iwapo upinzani utaamua kutangaza matokeo yake kabla ya matokeo rasmi ya IEBC, jambo linalohofiwa kwamba huenda likazusha mzozo wa kisiasa nchini.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: