Chama kikubwa cha wafanyikazi nchini Afrika Kusini, Cosatu kimeunga mkono kauli ya wale wanaomtaka rais Jacob Zuma kujiuzulu.
Japo Cosatu kinajulikana kuunga mkono chama tawala ANC, kimemshutumu rais Zuma kwa kile wanachokitaja kuwa na uhusiano wa karibu mno na familia moja ya jamii ya Wahindi huko Afrika Kusini, waitwao Gupta, wanaodaiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika serikali ya Zuma.
Bw. Zuma na falimia hiyo ya Guptas, wamekana kufanya kosa lolote.
Wiki iliyopita chama chengine mshirika wa ANC The South African communist party pia kilimtaka Bw. Zuma kung'atuka mamlakani kutokana na kashfa tele zinazozidi kumuandama, madai ya makosa ya ufisadi.
Sarafu ya Rand imekuwa ukiyumba yumba kutokana na malumbano hayo ya kisiasa nchini Afrika Kusini hasa tangu kufutwa kazi kwa aliyekuwa waziri wa fedha nchini humo Pravin Gordhan.
0 Post a Comment:
Post a Comment