9 Mei 2017
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, Fatou Bensouda amesema timu yake inakusanya ushahidi wa makosa yanayodaiwa kutendewa wahamiaji wanaopitia nchini Libya.
Amesema wahamiaji hao pia wamekuwa wakibakwa kuuawa na kuteswa.
Fatou Bensuda ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Libya imeonekana kuwa soko la usafirishaji haramu wa binadamu ambapo maelfu ya wahamiaji wasio na msaada, wakiwemo wanawake na watoto wamekuwa wakishikiliwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Amesema vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa matukio ya mauaji, ubakaji na utesaji yamekuwa ni matendo ya kawaida katika eneo hilo.
Mahakama hiyo ya ICC inachunguza iwapo makosa hayo yataangukia kwenye makosa yanayohukumiwa na mahakama hiyo.
Mahakama hiyo tayari inataka kushughulikia kesi dhidi ya mkuu wa usalama wa zamani wa Kanali Muammar Gaddafi Al-Tuhamy Mohamed Khaled ambaye anakabiliwa na tuhuma za kutekeleza makosa ya uhalifu wa kivita.
0 Post a Comment:
Post a Comment