Polisi nchini Kenya wanafanya uchunguzi kubaini iwapo kijana mmoja alijiua baada ya kushiriki mchezo wa mtandaoni, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Mkuu wa polisi wa Nairobi Japheth Koome amesema wanachunguza taarifa kwamba kijana wa miaka 16 alijitoa uhai kutokana na mchezo huo.
Kituo cha Centre for Safe Internet cha Bulgaria kinasema kufikia sasa hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha vifo vilivyotokana na kucheza mchezo huo.
Mchezo huo unadaiwa kuwapa changamoto washriiki wafanya mambo ya kutisha, ambapo jambo la mwisho linakuwa ni kujitoa uhai.
Taarifa kuhusu mchezo huo vimeripotiwa nchini Brazil na Urusi lakini hakuna visa vyovyote vya watu kujitoa uhai ambavyo vimethibitishwa rasmi kwamba vilitokana na mchezo huo kufikia sasa.
0 Post a Comment:
Post a Comment