Shkuba na wenzake watinga Marekani wanakokabiliwa na kesi ya dawa za kulevya


4 Mei 2017

 Mtuhumiwa wa usafirishaji wa madawa ya kulevya Ali Khatib Haji “Shkuba” na washirika wake wawili, Iddy Salehe Mfullu na Tiko Emanual Adam wamewasili Marekani kwa ajili ya kukabili mashtaka ya  kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya litakalosikilizwa  katika Mahakama Kuu Houston, Texas.
Watuhumiwa hao watatu waliwasili nchini Marekani jana (Jumanne) baada ya kesi hiyo kukubaliwa kusikilizwa nchini humo
Itakumbukwa kuwa Machi 2016, Jopo la maafisa mashtaka (grand jury) la Huston, Texas, lilipitisha mashtaka dhidi ya Shkuba na washirika wake kwa tuhuma za kula njama ya kumiliki kwa lengo la kusambaza madawa ya kulevya aina ya heroin nchini Marekani katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015.
Hatimaye Serikali ya Marekani iliwasilisha ombi rasmi kwa Tanzania la kuwapeleka watuhumiwa hao watatu nchini Marekani.
“Kesi hii ni mfano mzuri sana wa jinsi tunavyoweza kuimarisha usalama wa kikanda na kimataifa pale tunapofanya kazi pamoja,” amesema Virginia Blaser, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania).
Mwaka 2014 Shkuba alitiwa mbaroni na Serikali ya Tanzania kwa tuhuma za usafirishaji madawa ya kulevya baada ya msako wa miaka miwili uliofuatia kukamatwa kwa takriban kilo 210 za dawa za kulevya aina ya heroine mkoani Lindi,  Januari 2012.
Machi 9, 2016, Ofisi ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ya Wizara ya Fedha ya Marekani (U.S. Department of the Treasury’s Office of Foreign Assets Control - OFAC) chini ya sheria ya kuwabainisha raia wa kigeni walio vinara wa biashara ya madawa ya kulevya (Foreign Narcotics Kingpin Designation Act – Kingpin Act) ilimtaja Hassan na kundi lake kama raia wa kigeni aliye kinara wa biashara hiyo haramu.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: