Vijana Mwanza waandaliwa mazingira bora


   


Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela  


Vijana wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili kurahisisha utekelezaji wa sera ya kuwawezesha na kuwawekea mazingira bora ya kujiajiri.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk Leonard Masale ametoa wito huo hivi karibuni alipozindua mafunzo ya siku tano ya ufugaji kuku wa kienyeji yaliyodhaminiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), Kanda ya Ziwa kwa ajili ya vijana kutoka wilayani humo.
“Serikali iko tayari kuandaa mazingira bora ya kuwezesha vijana kuanzisha na kuendesha shughuli za ujasiriamali katika maeneo yao. Kazi hiyo itakuwa rahisi zaidi vijana wakijiunga kwenye vikundi,” alisema Dk Masale.
Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Ziwa, Hildegardis Bitegera amesema mafunzo hayo yanalenga kuboresha ujuzi na kuwapa washiriki mbinu mpya za ufugaji wenye tija badala ya kufuga kwa mazoea.


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: