Kenyatta aongeza mshahara wa chini Kenya


  • 1 Mei 2017
Rais Kenyatta amesema kuwa hatua za kuboresha uchumia ili kuwawezesha wakenya kuishi maisha mema zinaendelea.
Rais Kenyatta amesema kuwa hatua za kuboresha uchumia ili kuwawezesha wakenya kuishi maisha mema zinaendelea.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza nyongeza ya mshahara wa chini zaidi mfanyakazi anastahili kulipwa kwa asilimia 18.
Rais Kenyatta alitangaza hilo wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani iliyoandaliwa katika bustahi ya Uhuru mjini Nairobi
Hadi shilingi 100,000 za marupurupu na malipo ya kufanya kazi saa za ziada hazitatozwa kodi kama njia ya kuwapunguzia wakenya gharama ya kupanda kwa maisha.
Nao mshahara ulio chini ya shilingi 13,475 hautatozwa kodi.
Rais Kenyatta amesema kuwa hatua za kuboresha uchumia ili kuwawezesha wakenya kuishi maisha mema zinaendelea.
Amesema kuwa jitihada za sasa za ujenzi wa barabara, kuondoa vizuizi vya kufanya biashara na elimu bora ni baadhi ya hatua.
Kenyatta amesema shilingi bilioni 40 zimedhinishwa kwa ujenzi wa mji wa kiteknolojia wa konza
Image captionKenyatta amesema shilingi bilioni 40 zimedhinishwa kwa ujenzi wa mji wa kiteknolojia wa konza
Rais amewataka waajiri kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanahudumu katika mazingira salama na kuongeza kwa serikali itaanzisha zoezi la kukagua usalama katika maeneo ya kazi.
Huku Kenya ikielekea kwenye uchaguzi mkuu rais Kenyatta amewataka wakenya kutojihusisha na ghasia akisema kuwa amani ndicho kigezo cha maendeleo ya nchi.
Kenyatta amesema shilingi bilioni 40 zimedhinishwa kwa ujenzi wa mji wa kiteknolojia wa konza. Amesema ujenzi wa mji huo utabuni nafasi za ajira 16,000 wakati ukijengwa na zingine zaidi ya 200,000 utakapokamilika kujengwa.
Rais Kenyatta pia amewashauri wakenya kufanya kazi na mashirika yaliyothibitishwa tu wakati wanatafuta kazi nchi za ng'ambo hasa Mashariki ya Kati.
Kwa upandE wake katibu mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini Kenya Francis Atwoli Ametaka kubuniwa miji zaidi kwa lengo kupunguza msongamano kwenye mji wa Nairobi na kubuni nafasi za ajira.
 Mshirikishe Mwenzako: zakacheka.blogspot.com/ www.zakacheka.simplesite.com +255 625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: