Milio ya risasi yasikika kambi za jeshi Ivory Coast


12 Mei 2017

Barabara nyingi za miji zimebaki bila watu
Barabara nyingi za miji zilibaki bila watu
Milio ya risasi imetanda angani katika kambi za kijeshi nchini Ivory Coast, baada ya wanajeshi waliojaa hamaki na hasira nchini humo, kuanza kufyatua risasi angani, huku wakifunga barabara za kuingia na kutoka katika miji kadha ya nchi hiyo.
Miji ya hivi punde zaidi kukumbwa na machafuko hayo ni pamoja na ule wa Bondoukou na Man.
Kwa sasa wizara ya ulinzi katika mji ulioko pwani wa Ivo, inasema kuwa wanakamati wa baraza kuu la usalama wa taifa, wanafanya mkutano wa dharura ili kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Wanajeshi hao wanalalamikia tangazo la ghafla kwamba, wameachia azma yao ya kuishinikiza serikali kuwalipa fidia kwa kuachana na vita na badala yake kujiunga tena na serikali.
Milio ya risasi inasikika katika makao makuu ya jeshi mjini Abidjan, na pia katika mji wa pili kwa ukubwa wa Bouake.
Aidha ghasia kama hizo zinashuhudiwa katika miji ya Korhogo na Odienne kaskazini mwa nchi.
Ivory Coast
Wanajeshi hao wanasemekana kupandwa na hamaki kwamba, hawakushauriwa, kabla ya tangazo lililotolewa na msemaji wa kundi hilo, Sajini Fofana, akimuomba msamaha Rais Alassane Ouattara kwenye sherehe iliyotangazwa kwa runinga moja kwa moja katika mji mkuu wa Abidjan, hafla iliyodhamiriwa kumaliza rasmi malalamiko na uhasama huo.
Mnamo mwezi Janauri maelfu ya wanajeshi waasi, wengi wao waliokuwa wanachama wa kundi la waasi, waliilazimisha serikali ya nchi hiyo kuwalipa marupurupu ya dola elfu nane kila mmoja.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: