Aliyekuwa nyota wa mchezo wa miereka Marekani Dwayne Johnson maarufu 'The Rock' anataka kuwania urais nchini humo.
Katika mahojiano na jarida la GQ, nyota huyo wa uigizaji anasema kuwa amelifikiria sana wazo hilo.
Anasema kwamba iwapo angekuwa rais ingekuwa muhimu.
''Uongozi ni muhimu. Kuchukua jukumu la kila mtu''.
Lakini Johnson sio nyota pekee mwenye maono ya kutaka kuhamia katika ikulu ya Whitehouse 2021.
Mark Zuckerberg , bilionea na mkurugenzi wa mtandao wa facebook pia huenda ana ndoto kama hiyo.
Amekuwa na mpango wa kuwatembelea raia wote wa Marekani katika majimbo 50 na amekuwa akipeperusha hewani ziara zake moja kwa moja katika mtandao wa facebook hatua ambayo inaokena kuupigia debe mtandao huo.
Mark Zuckerbag
Pia kumekuwa na picha za urais kama vile kupeleka tinga kuwaosha watoto wa ng'ombe na hata kwenda kanisani kwa kuvalia koti badala ya nguo zake za kawaida.
Jay Z huenda alishindwa kumsaidia Hillary Clinton kushinda uchaguzi wa Marekani, lakini hiyo haimaanishi kwamba hatowania urais.Msanii wa muziki Jay Z, na mkewe Beyonce wakati wa kampeni za Hillary Clinton
Duru ziliambia jarida la Radar kwamba Jay Z ana mpango wa kuwania wadhfa wa kisiasa mjini New York na Beyonce anamuunga mkono mumewe asilimia 100 kwa 100.
Aliambia Newsbeat mnamo mwaka 2010 kwamba anatamani angekuwa rais.
Iwapo nyota yako ni kumuona Kim Kardashian kuwa mke wa rais basi utalazimika kusubiri kiasi.
Hiyo ni kwa sababu Kanye West ameamua kusubiri hadi 2024 kuwania Urais.
Alikuwa ametangaza kwamba angewania 2020 lakini baada ya kukutana na rais Donald Trump mwaka uliopita aliamua kutompinga katika kipindi chake cha pili.
Katika chapisho la mtandao wa Twitter ambalo lilifutwa alisema: Wasanii wa muziki wa Rap ni wanafilosofia wa wakati huu, watu maarufu ni washawishi wetu wa sasa ,mwangalieni rais hakuwa katika siasa na alishinda.
0 Post a Comment:
Post a Comment