Mvua yaharibu barabara kuu Bukoba na Mwanza


13 Mei 2017


Mvua ilisababisha barabara kuu ya Mwanza -Bukoba kukatika eneo la Kemondo, hivyo magari ya abiria na mizigo kuzunguka Kyetema kupitia Katerero kutokea Muleba.
Barabara hiyo imekatika jana (Ijumaa) saa 11:00 alfajiri kutokana na mvua iliyonyesha usiku kucha na kusababisha maji kujaa kwenye karavati.
Kutokana na hali hiyo wananchi na hasa wafanyabiashara wa eneo la Kemondo walishindwa kuendelea na shughuli zao kwa kukosa mawasiliano.
Naima Issa, mkazi wa Kemondo alisema wanafunzi walikatisha masomo baada ya kukosa eneo la kupita.
Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Kagera, Andrew Kasamwa alisema watumiaji wa barabara hiyo walianza kutumia njia mbadala kwa kupita Katerero mzunguko wa umbali wa takriban kilomita 10.
Alisema jitihada zinafanywa kukarabati eneo hilo ili kurejesha mawasiliano.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: