5 Mei 2017

Mwanamke raia wa Misri aliyetambulika kuwa mtu mzito zaidi duniani amelazwa katika hospitali moja mjini Abu Dhabi ili kuendelea na matibabu.
Eman Abd El Aty anayedaiwa kuwa na kilo 500 aliondoka hospitali ya India siku ya Alhamisi baada ya madaktari kusema kuwa amepoteza takriban kilo 250.
Alisafirishwa kupitia ndege ya abiria hadi UAE
Madaktari wanasema kwamba atafanyiwa matibabu ya viungo.
Katika majuma ya hivi karibuni kulizuka ugomvi kati ya madaktari wake India na familia yake.

Ugomvi huo ulianza baada ya dadake Shaimaa Selim kutoa kanda ya video katika mtandao wa kijamii kwamba dadaake alikuwa bado hawezi kuzungumza ama hata kutembea na kwamba hakupoteza kilo nyungi kama ilivyoarifiwa na hospitali hiyo.
Hospitali hiyo ilikana madai hayo.
Bi Selim alitaka dadake kusalia katika hospitali hiyo hadi atakapoanza kutembea, lakini madaktari wa mifupa katika hospitali hiyo walisema kuwa hatotembea tena.
Madaktari na wauguzi waliandamana na mwanamke huyo hadi Abu Dhabi kulingana na ripoti.

Alikuwa amewasili nchini India kwa kutumia ndege ya kubeba mizigo mnamo mwezi Februari na akawa akiwekwa maji pekee ili kupunguza uzani wake ili madaktari waweze kumfanyia upasuaji wa kupunguza tumbo lake.
0 Post a Comment:
Post a Comment