TTCL kuzima mitambo yote ya CDMA


7 Mei 2017
 

 Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo saa 7.00 itahitimisha mchakato wa kuzima huduma ya simu za mkononi zinazotumia teknolojia ya CDMA.
Mchakato huo ulianza kutekelezwa tangu Januari mwaka huu na unahitimishwa leo usiku.

Kwa mujibu wa taarifa TTCL iliyotolewa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Waziri Kindamba, ni kuwa uzimaji huo utaenda sambamba na kuwapatia wateja wao huduma mbadala kwa kutumia teknolojia ya 3G na 4G-LTE yenye ufanisi wa viwango zaidi.
Kampuni imeomba radhi kwa wateja wake kutokana na usumbufu utakaojitokeza na kuwataka wawasiliane na kituo cha huduma kwa wateja kilichopo karibu nao kwa msaada zaidi.
“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza wakati wa zoezi hili linalolenga kuboresha huduma kwa wateja wetu,” amesema Kindamba kwenye taarifa hiyo.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: