Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in ameapishwa rasmi
Rais mpya wa Korea Kusini, Bwana Moon Jae-In, ameanza kazi rasmi afisini kwake baada ya kuapishwa.
Bwana Moon ametoa wito kupunguza uhasama kati ya Korea Kusini na Kaskazini na wakati huohuo kutaka kujua ni kwa nini Marekani iliweka makombora ya Ulinzi katika ardhi ya nchi yake.
Amesema kuwa angependelea kutembelea Pyongyang katika hali nzuri.
Wakili huyo wa haki za kibinaadamu anayejulikana kwa maoni yake huria anataka kuimarisha uhusiano na Korea Kaskazini kinyume na sera iliopo kwa sasa.
Pia ameapa kuliunganisha taifa hilo linalokabiliwa na ufisadi ambao ulisababisha mtangulizi wake kushtakiwa mbali na kuimarisjha uchumi.
Bwana Moon aliapishwa kuwa rais wa 19 wa Korea Kusini na kujaza pengo lililowachwa wazi na Park Geun hye.
Mwanachama huyo wa chgama cha Democrat amejionyesha kuwa mtu ambaye anaweza kuliendesha mbele taifa hilo kutoka kwa ufisadi mbali na kuliunganisha.
Pia amekosoa mamlaka ya hapo awali kwa kushindwa kuzuia utengenezaji wa silaha wa Norea Kaskazini na ameapa kuimarisha uchumi na kuangazia tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana ambalo ndio tatizo kubwa la wapiga kura
Uongozi wa bwana Moon utaangaliwa huku kukiwa na wasiwasi mwingi katika eneo hilo.
Marekani na Korea Ksakazini zimekabiliana kimaneno katika majuma ya hivi karibuni baada ya Pyongyang kufanya majaribio ya makombora.
0 Post a Comment:
Post a Comment