Salva Kiir amfukuza mkuu wa majeshi


10 Mei 2017

Rais Salva Kiir
Rais Salva Kiir
Rais Salva Kiir wa Sudan kusini amemfukuza kazi mkuu wa Jeshi la nchi hiyo Jenerali Paul Malong.
Hakuna sababu yoyote iliyotajwa katika vyombo vya habari vya serikali, lakini katika siku za hivi karibuni maafisa wengi wa ngazi za juu wamekuwa wakijiuzulu na pia wengine kutoka serikali ya Sudan Kusini.
 Jenerali Malong anaonekana na Wasudan wengi kama mtu mwenye nguvu, na wanasubiri kuona atakavyopokea kuondolewa katika nafasi hiyo.
Wengi wamekuwa na wasiwasi kuhusiana na upendeleo wa kikabila na uhalifu wa kivita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo yameiingiza Sudan kusini katika mgogoro uliodumu kwa miaka minne sasa.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: