Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio hilo lilitokea Mei 10, saa moja jioni baada ya bibi kumchapa viboko mjukuu wake akimtuhumu kuchelewa kurudi nyumbani alipoenda kucheza nyumba jirani.
Msangi amesema mtoto huyo Balangi Mika aliporejea nyumbani bibi yake alimkamata na kumchapa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake na kusababisha kifo chake.
Amesema bibi huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na utakapokamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu mashtaka.
0 Post a Comment:
Post a Comment