Siku ya wafanyakazi duniani haikua na mwisho mwema nchini Venezuela baada ya kutokea vurugu na maandamano mara baada ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro kuhutubia taifa akitangaza kuundwa kwa Bunge jipya ili kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Rais Maduro, alitoa wito wa kuundwa kwa kwa Bunge la katiba ambalo litakuwa na mamlaka ya kuandika katiba mpya,kwa madai kuwa chombo hicho kipya kitaundwa na raia wa kawaida,na kuachana na bunge la kitaifa linalodhibitiwa na upinzani
Hata hivyo kiongozi wa Upinzani, nchini humo, Henrique Capriles amesema chombo hicho kipya kitakuwa kina malengo ya kuhujumu katiba .
Bunge la kitaifa limekuwa likitaka Rais Maduro ajiuzulu wakati taifa hilo likikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi.
0 Post a Comment:
Post a Comment