Wanaharakati watano watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja wamekamatwa na kuziliwa mjini Moscow.
Walikamatwa walipokuwa wanaelekea kwa afisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Urusi kuwasilisha malalamiko.
Polisi wamesema watano hao wamekamatwa kwa sababu shughuli hiyo yao haikuwa imeidhinishwa.
Walioakamtwa ni raia wanne wa Urusi na mmoja wa Italia.
Wanaharakati hao walisema watu zaidi ya milioni mbili walikuwa wametia saini ombi la kuitaka serikali ichunguze tuhuma za kuteswa na kuzuiliwa kwa wapenzi wa jinsia moja katika jimbo la Chechnya nchini Urusi.
Maafisa wa Chechnya wamekanusha madai kwamba hata kuna wapenzi wa jinsia moja nchini humo.
Wiki iliyopita, rais wa Urusi Vladimir Putin aliunga mkono uchunguzi kuhusu operesheni ya kuwasaka wapenzi wa jinsia moja Chechnya.
Mapema mwezi huu, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliihimiza Urusi kulinda haki za wapenzi wa jinsia mnamo.
0 Post a Comment:
Post a Comment