3 Mei 2017
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hana tatizo baada ya kuzomewa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wafanyakazi akisema kuwa nchi hiyo ni ya demokrasia na wala sio ya kiimla.
"Utakubali kuwa nchi yenye viongozi wa kiimla, hakutakuwa na maandamano wala kuzomea," bwana Zuma aliwaambia waandishi wa habari.
Katika nchi isiyo na demokrasia, kutakuwa na rais mwenye hasira akiamrisha polisi kuwakamata watu hawa.
Wafanyakazi walimkemea Bwana Zuma na kumtaka ajiuzulu.
Akijibu, bwana Zuma alisema, "Nina furaha sana kuwa watu wa Afrika Kusini wamekomaa kidemokrasia na wana rais ambaye wanaweza kumzungumzia chochote walicho nacho akilini mwao."
Alionekana kupuuzilia mbali uwezekano wa kuondoka madarakani, akisema kuwa katika nchi yenye demokrasia viongozi hupigiwa kura kuingia na kuondoka madarakani.
Bwana Zuma amekuwa chini ya shinikizo kutoka kwa makundi kadha vikiwemo vyama vya wafanyakazi, biashara kubwa, vyama vya upinzai na wanachama wa chama chake.
Ameandamwa na sakata za ufisadi wakati wa kipindi chake na kuzua shutuma baada ya kumfuta waziri wake wa fedha aliyekuwa akiheshimiwa mnamo mwezi Machi.
Bwana Zuma anasema hajafanya lolote baya.
0 Post a Comment:
Post a Comment