Rais Trump achukizwa na tuhuma za Comey



9 Juni 2017

Comey
Rais Trump na aliyekuwa mkurugenzi wa FBI,James Comey
Rais Trump pamoja na timu yake wamejibu vikali dhidi ya tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa mkurugenzi wa FBI ,kuwa rais Trump alimtaka kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama na Urusi.
Hapo jana James Comey alihojiwa na Kamati ya Bunge la Seneti ya Usalama na kumtupia lawama Rais Trump kwa kuingilia uchuguzi unamhusu kujihusisha na Urusi.
Wakili binafsi wa rais Trump,Marc Kaswitz amepinga vikali shutuma hizo zilizotolewa na Comey na kudai kuwa huo ni uzushi.
"Raisi hakuwahi kutoa maelekezo au mapendekezo kwa Comey kuacha kumchunguza wa mtu yeyote ".
Rais Trump pia alitoa mustakhabali wake juu ya suala hili;
"hakuna kitu chenye dhamani ambacho kinakuja kiurahisi,lakini tunajua jinsi ya kupambana vizuri zaidi mtu mwingine yeyote na hatutakata tamaa .Sisi ni washindi na tunaenda kupambana na kushinda na tutakuwa na mustakabali ambao hauelezeki kwa siku za mbeleni,na tutaenda kuwa pamoja
Comey katika ushaidi alioutoa alieleza namna ambavyo alijisikia vibaya mara baada ya rais Trump kumtaka kuachana na uchunguzi huo wa mshauri wa zamani wa masuala ya usalama na juu ya urusi.
Na anaona ndio sababu ilionekana haendani na majukumu ya shirika la kijasusi la FBI


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: