1 Agosti 2017
Julius Malema amuita Rais Edgar Lungu dikteta
Serikali ya Zambia imejibu vikali matamshi ya kiongozi wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema, akisema kuwa Rais wa Zambia Edga LUungu ni muoga.
Mwishoni mwa wiki bwana Malema ambaye ni kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), pia alimuita bwana Lungu kuwa yeye ni dikteta ,akimfananisha na viongozi wa utawala wa ubaguzi wa rangi.
Matamshi yake yanakuja baada ya kukamatwa kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, kufuatia mzozo kuhusu msafara wa Rais Lungu. Kwa sasa Hichilema anakabiliwa na mashtaka ya uhaini.
Msemaji wa serikali ya Zambia Kampamba Mulenga, anasema kuwa mauaji hayo hayana msingi wowote na kuwa Zambia ni nchi iliyokomaa kisiasa yenye uwezo wa kutatua masuala yake ikiwa yapo.
0 Post a Comment:
Post a Comment