Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini Kenya kufanyika, Tanzania imeshuhudia wimbi kubwa la wageni kutoka nchini Kenya hasa katika miji ambayo iko karibu na mpakani kama vile Tanga na Arusha .
Wandishi wetu Aboubakar Famau ambaye alikuwa mjini Tanga, alikutana na baadhi ya wageni hao ambao baadhi walidai wameingia Tanzania kwa ajili ya matembezi huku wengine wakikiri kwamba wafika nchini humo wakihofia huenda baada ya uchaguzi kukatokea machafuko kama ilivyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
"Mimi sijakimbia uchaguzi. Nimekuja kwa ajili ya matembezi kwa sababu ndio nimepata fursa wakati huu," alisema Sumeiyan Sharif akiwa safarini kutoka Mombasa kuelekea jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Sumeiya aliongeza kusema kuwa, ni kweli watu wingi wamesafiri kama moja wapo ya tahadhari kwa kuhofia lolote linaweza kutokea.
Fursa za Kiuchumi
Licha ya mji wa Tanga kuwa karibu na mpaka wa Kenya, mara nyingi mji huo unakuwa hauna pilka pilka za kibiashara kama ilivyo katika mikoa mingine ya Tanzania.
Hata hivyo, yale maneno ya wahenga ya mgeniaje mw enyeji apone yanaonekana kuanza kuleta maana kwa wakazi wa Tanga hasa vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa pikipiki maarufu kama bodaboda.
Ali Kijoka ambaye ni dereva wa bodaboda anasema wageni hao wameleta ahueni ya maisha.
"Tunashukuru wageni wanavyokuja kama hivi hali ya maisha nayo inabadilika. Angalau tunapata abiria na hoteli nazo zinajaa. Angalau watoto wanapata chakula," amesema Ali Kijoka kutoka maeneo ya kituo cha mabasi mjini huko.
Athari za watu kukimbia uchaguzi.
Katika zoezi lolote la upigaji kura, idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura ndio inayoweza kuleta mabadiliko ya uongozi. Hivyo mara nyingi, wapiga kura wanapokimbia upigaji kura, hawamsaidii mtu wanayemtaka kuingia madarakani.
"Tatizo ni woga. Wanaogopa kumchagua mtu wanaemtaka. Lakini wanashindwa kujua hata kura 10 zikipotea itamwathiri mtu ambae wanamtaka kumpa uongozi," ameelezea Hamad Khalfan Singano, dereva wa Tahmeed Coach.
Watu wa Tanga na Mombasa wamekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kidugu.
Mbali na mwingiliano wa kibiashara, lakini pia kabila la wadigo linapatikana katika nchi mbili hizo kupitia mipaka ya Horo Horo na Lunga Lunga.
Nijuze habari kwa 0625 966 236
0 Post a Comment:
Post a Comment