27 Sep 2017
Mtandao wa kijamii wa Twitter umetangaza jaribio lake la kongeza idadi ya maneno ya ujumbe ambayo mtu anaweza kuandika kwenye mtandao huo kwa mara moja hadi kufikia 280 ambayo ni mara mbili ya kiwango cha idadi ya maneno yaliyopo kwa sasa.
Mtandao huu ambao umekuwa na idadi ya zaidi watumiaji milioni mia tatu,umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya ukuaji na hivyo inatafuta namna mbalimbali za kukuza wigo wa watumiaji.
Kundi dogo la watumiaji wa mtandao huo watahusishwa katika jaribio hilo la kuongeza idadi ya maneno ya kuandika.
Kampuni hiyo imesema hiyo ni hatua ya kutatua moja ya changamoto ambayo imekuwa ikiwasumbua watumiaji wengi.
0 Post a Comment:
Post a Comment