KAMPUNI YA BARRICK GOLD KUILIPA TANZANIA HISA 16% NA MGAWO WA 50%

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.
19 Oktoba 2017

Barrick Gold imekubali kulipa Serikali ya Tanzania hisa ya asilimia 16 na mgawo wa asilimia hamsini


Kampuni ya inayomiliki migodi ya madini nchini Tanzania, Barrick Gold imekubali kuilipa Serikali ya Tanzania hisa ya asilimia 16 na mgawo wa asilimia hamsini ya mapato ya mauzo ya dhahabu kutoka migodi 3 inayoimiliki.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria mpya za madini ya Tanzania baada ya kampuni hiyo kukubali kuwa na mazungumzo na Serikali ya Tanzania .
Vilevile kampuni hiyo imekubali kutoa Dola za Kimarekani milioni 300 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kutokana na biashara ya kampuni hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo,Prof. Thornton amesema Barrick Gold Corporation watazingatia makubaliano haya na wanaamini kuwa yamefungua ukurasa muhimu utakaowezesha kufanya biashara kisasa.
Kwa upande wake Rais wa Tanzania John Magufuli amesema makubaliano hayo yataisaidia nchi kuzalishaji ajira zaidi, kupata manufaa mbalimbali yanayostahili ikiwemo fedha za kugharamia huduma za kijamii kwa wananchi na yanajenga msingi imara ambao utaiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake za madini.
Wakati huohuo waziri wa Katiba na Sheria nchini humo Prof.Palamagamba Kabudi ambaye alikuwa kiongozi wa mjadala huo amesema sheria hiyo iliyopita mwezi july imeleta dira mpya katika biashara hiyo ya madini.
FACEBOOK: zakacheka.blogspot.com na download App yetu huko
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: