30 0ktoba 2017
Makinda waliopikwa kwenye vituo vya michezo vya kulea vipaji vya soka vya Chelsea na Manchester City wametajwa kuibeba England ilipotwaa taji la Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17.
Kikosi hicho cha England kilijaa nyota ambao wamepikwa katika klabu za Chelsea na Manchester City lakini wachezaji hao hawapo tayari kuzichezea timu hizo.
England ilipata ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Hispania, huku wakifuata nyayo za kaka zao vijana wenye chini ya umri wa miaka 20 walionyakua Kombe la mwezi Juni mwaka huu walipowalaza Venezuela kwa bao 1-0.
Mchezaji Rhian Brewster aliibuka na kiatu cha dhahabu baada ya kutangazwa kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo.
0 Post a Comment:
Post a Comment