Zitto Kabwe aachiwa kwa dhamana

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM
31 OKTOBA 2017
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe akitoka kituo cha polisi Kamata,mjini Dar es salaam
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe akitoka kituo cha polisi Kamata,mjini Dar es salaam     

Zitto Kabwe , kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT Wazalendo, ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa mara mbili siku ya leo kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi.
Mbunge huyo wa Kigoma mjini anatakiwa kuripoti kituo cha polisi siku ya Jumanne wiki ijayo, kisha kupandishwa mahakamani kwa makosa mawili tofauti ikiwepo kutoa takwimu za uongo na makosa ya sheria za kimtandao.
Mbunge huyo wa Kigoma mjini, alikamatwa mara ya kwanza asubuhi ya Jumanne nyumbani kwake mjini Dar es salaam na kupelekwa kituo cha polisi Chang'ombe.
Baada ya masaa kadhaa mbunge huyo aliachiliwa huru kabla ya kukamatwa tena kwa maelekezo ya ofisi ya afisa upelelezi makosa ya jinai.
Akizungumza na BBC awali , wakili wa Bwana Kabwe, Stephan Ally Mwakibolwa anasema sababu zilizotajwa kwa kushikwa kwake mara ya kwanza ni kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi.
"Kauli kubwa haswa wanayosema ni kuihusisha serikali ya CCM na matukio ya watu waliookotwa katika fukwe za bahari ya hindi wakiwa wamefariki ,pamoja na tukio la mbunge Tundu Lissu"alisema
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER Zakacheka News Line

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: