Uhuru Kenyatta amtaka Raila Odinga kwenda mahakamani

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM
31 OKTOBA 2017

Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa upinzani Raila Odinga
Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa upinzani Raila Odinga

Rais Uhuru Kenyatta amepinga kufanyika kwa mazungumzo yoyote na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Kenya uliosababishwa na uchaguzi mkuu uliokwisha.
Katika hotuba yake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio , rais Kenyatta amesema kuwa mpinzani wake mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kwa mara nyengine tena kupinga uchaguzi wake.
Kenyatta amewataka wapinzani wake wa Nasa kutumia njia zote za kisheria katika kupigania haki yao.
Wawacheni mwanzo watumie njia zote za kisheria zilizosalia wawacheni wafanye wanachotaka.
Hakuna mtu yeyote atakayewadhulumu haki yao ya kikatiba.
''Kuhusu ajenda yangu ya kusonga mbele nitazungumza baada ya makabiliano ya mahakamani yamekwisha'' , alisema Kenyatta katika makao makuu ya tume ya uchaguzi katika eneo la Bomas jijini Nairobi.
Rais Kenyatta pia alimshutumu Raila Odinga kwa kujiondoa katika uchaguzi huo.
''Licha ya kwamba mpinzani wangu mkuu alienda mahakamani akitaka uchaguzi wa urais kufutiliwa mbali na akakubaliwa, aliamua kutotilia maanani uamuzi wote kwa pamoja ambao uliagiza kufanyika kwa uchaguzi katika kipindi cha siku 60 uliosimamiwa na IEBC.Baadaye alikaataa kushiriki katika uchaguzi''.
Katika uchaguzi wa marudio Uhuru alijipatia kura 7,483,895 huku Raila Odinga akijipatia kura 73,228 hata baada ya kujiondoa katika uchaguzi huo.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER Zakacheka News Line

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: