Tutashinda tuition centre iliyoko Mjini Mwanza,inayofundisha masomo kwa shule za Msingi(Pre&Primary Schools) inatafuta eneo la kufundishia jijini Mwanza. Kwa ambaye anaeneo lililowazi na yuko tayari kutusaidia awasliane nasi kwa sms kwa Simu namba 0621261295.
Ahsante.
Badhi ya wajeruhi wakipata matibabu katika hosipitali ya Rulenge, Ngara
a Wanafunzi sita wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na wengine 41 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu wakicheza.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Oromi huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.
Mkoa wa Kagera ni eneo linalowahifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani kama Burundi. Baadhi ya wakimbizi hao walikuwa wanajeshi ambao waliacha silaha zao katika baadhi ya makambi.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Oromi amesema tayari timu ya upelelezi imetumwa katika eneo hilo kuchunguza sehemu ambapo bomu lililipukia.
Haki miliki ya pichaWatoto wakipata huduma katika hosipitali ya Rulenge baada ya mlipuko
Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rulenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.
"Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata majeraha, wengine wameumia macho." Dokta Mariagoreth ameiambia BBC.
Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea.
Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!
0 Post a Comment:
Post a Comment