Jeshi la Israel limesema mashambulizi yake roket yanazilenga ngome tatu za kijeshi za wapiganaji wa kundi la Hamas,ikiwa ni hatua ya kujibu shambulizi dhidi yao la kutoka ukanda wa Gaza.
Israel pia imeamuru kufungwa kwa mpaka kati yake na Gaza,baada ya shambulizi la nne maroketi yanayodaiwa kurushwa na kundi la HAMAS.
Hali hii ya mapigano ya kundi la Hamas inadaiwa kuwa ni kutokana na hasira kufuatia hatua ya rais Trump kuutambua mji wa Jesrusalem kama makao makuu ya Israel.
Hata hivyo jeshi la Israel linasema kuwa makombora kati ya yaliyorushwa,walifanikiwa kuyazuia,ambapo moja lilianguka eneo la wazi kusini mwa Israel na jingine lilipoteza uelekeo.
•Tuma habari picha na video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
0 Post a Comment:
Post a Comment