Miili ya wanajeshi waliouawa DRC yarejeshwa Tanzania

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania waliouawa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Miili hiyo imesafirishwa kwa ndege za Umoja wa Mataifa kutoka nchini DR Congo.
Waliuawa wakati wa shambulio lililotekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Wanajeshi wengine zaidi ya 50 walijeruhiwa.
Umoja wa Mataifa ulisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.
Waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alishutumu vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu wa kivita.

Miili ikitolewa kwenye ndege na wanajeshi
Image captionMiili ikitolewa kwenye ndege na wanajeshi

Aliitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika wanafaa kuwajibishwa.
Wanajeshi zaidi walitumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi.
Bw Guterres alisema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni.

Maafisa wakuu wa jeshi walikuwa uwanja wa ndege kuilaki miili hiyo
Image captionMaafisa wakuu wa jeshi walikuwa uwanja wa ndege kuilaki miili hiyo
Miili hiyo imesafirishwa kwa ndege ya Umoja wa Mataifa
Image captionMiili hiyo imesafirishwa kwa ndege ya Umoja wa Mataifa


Kubeba jeneza


Miili ikisafirishwa
Kusafirishwa kwa malori
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: