Kanisa la mhubiri Bushiri anayetengeza 'fedha za miujiza' lafungwa Botswana

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Taifa la Botswana limelifunga kanisa la muhibiri mmoja wa Malawi mwenye utata anayedaiwa ''kutembea angani''.
Serikali ilithibitisha kufungwa kwa kanisa la Bushiri la Christian Gathering Church ECG mjini Gaborone mara kadhaa kutokana na wasiwasi kuhusu ''fedha za miujiza''.
Chombo cha habari cha Malawi24 kimeripoti kwamba kanisa hilo lilipinga uamuzi huo mahakamani uliochukuliwa chini ya mwaka mmoja baada ya muhibiri huyo kupigwa marufuku kuingia nchini humo.
Alikuwa ametarajiwa kuhudhuria kongamano fulani.
Hatahivyo waziri wa Botswana Edwin Batshu alitangaza mnamo mwezi Aprili 2017 kwamba bwana Bashir ambaye sasa anaishi Afrika Kusini atahitaji Visa ili kuingia, licha ya raia wa Malawi kutohitaji kibali hicho kulingana na chombo cha habari cha AllAfrica.com
Serikali imetangaza kwamba kanisa hilo litafungwa kabisa, huku gazeti hilo la Botwana likipata barua ilioambia usimamizi wake kwamba kibali cha kuendesha kanisa hilo kimefutiliwa mbali.
Wasiliana nami kwa 0625966236
Pia tembelea blog hii kwa neno la Mungu: www.zakachekainjili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: