Kenyatta : Mkipiga kura nendeni nyumbani

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

Zachary Bequeker +255 625 966

 

Rais Kenyatta
Kenyatta ametoa hotuba yake ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne





Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa wapiga kura nchini humo kuondoka kwenye vituo vya kupigia kura na kwenda nyumbani baada ya kupiga kura.
Kiongozi huyo, katika hotuba kwa taifa kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne, amesema wananchi wanafaa kupiga kura kwa amani.
"Ombi langu ni kwamba tunapopiga kura, hebu tupige kura kwa amani na tukumbuke kama nilivyosema jana, kwamba baada ya kupiga kura yako, nenda nyumbani. Nenda kwa jirani yako," amesema.
"Bila kujali anatoka wapi, kabila lake, rangi au dini, jirani yako ni ndugu yako. Jirani yako ni dadako.
"Jinsi ulivyopiga kura haifai kwa vyovyote vile kuathiri au kubadilisha jinsi unavyohusiana na jirani yako.
"Msalimie kwa mkono, kuleni chakula pamoja na uwaambie 'hebu tusubiri matokeo' kwani Kenya itaendelea kuwepo kwa muda mrefu hata baada ya uchaguzi."
Muungano wa upinzani ulikuwa awali umewashauri wafuasi wake kutoondoka vituo baada ya kupiga kura 'kulinda kura'.
Lakini baadaye, muungano huo ulibadilisha wito wake na kuwashauri waondoke baada ya kupiga krua lakini warejee baadaye jioni.
Polisi wamewataka wananchi kuheshimu sheria ya kutokuwa karibu na vituo vya kupigia kura umbali wa mita 400 baada ya kupiga kura.
"Wazazi wetu walipigana ndipo tuwe na Kenya nzuri na maisha mazuri…bila kujali matokeo ya uchaguzi huu, ni lazima tuendelee kushikamana pamoja kama wananchi. Zaidi ya yote, tukatae kutishwa. Lazima tukatae ghasia au majaribio yoyote ya kutugawanya," amesema Bw Kenyatta.
Nijuze habari kwa 0625 966 238
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: