ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Mike Pence (kulia) ametangaza hayo baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pichani.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem kabla ya mwisho wa mwaka 2019.
Kuhamishwa huko kutatokea mapema kuliko ilivyotarajiwa Rais Donald Trump alipotangaza mwezi jana kwamba Jerusalem ndio mji mkuu wa Israel na kuagiza maandalizi ya kuhamisha ubalozi yaanze.
Bw Pence ametoa tangazo hilo akihutubia bunge la Israel.
Hotuba yake ilikatishwa kwa muda na kundi la wabunge Waarabu ambao walikuwa wanalalamikia hatua hiyo ya Trump ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Hadhi ya mji wa Jerusalem imekuwa sehemu kuu ya mzozo wa Waisraeli na Wapalestina.
Mwezi uliopita, Umoja wa Mataifa uliidhinisha azimio la kuitaka Marekani kubatilisha uamuzi wake wa kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Azimio hilo liliyataka "mataifa kujiepusha kufungua afisi za kibalozi katika Mji Mtakatifu wa Jerusalem".
Kwa nini Jerusalem inazozaniwa?
Mji huo una maeneo matakatifu ya dini tatu zenye kufuata imani ya Ibrahim - Uyahudi, Ukristo na Uislamu - sana maeneo mengi yanapatikana Jerusalem Mashariki.
Israel ilitwaa eneo hilo kutoka Jordan wakati wa vita kati ya nchi za Kiarabu na Israel mwaka 1967 na imekuwa ikiuchukulia mji wote kuwa mji wake mkuu ambao hauwezi kugawanywa.
Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa) na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu pamoja na Wapalestina wenyewe.
Kwa mujibu wa maafikiano wakati wa mazungumzo ya amani ya Wapalestina na Waisraeli ya 1993, hatima ya mji huo ilifaa kuamuliwa wakati wa hatua za mwisho za mazungumzo.UN
Hatua ya Israel kudhibiti Jerusalem yote haijawahi kutambuliwa kimataifa na nchi zote zina afisi za kibalozi Tel Aviv.
Tangu 1967, Israel imejenga makazi kadha ya Wayahudi na kuna takriban walowezi 200,000 wa Kiyahudi eneo hilo. Makazi haya yamekuwa yakishutumiwa na jamii ya kimataifa.
Mataifa yalivyopiga kura kuhusu Jerusalem UN
Mataifa tisa yaliyopinga azimio la Umoja wa Mataifa mwezi jana yalikuwa: Marekani, Israel, Guatemala, Honduras, visiwa vya Marshall, Micronesia, Nauru, Palau na Togo.
Mataifa 35 yalisusia kura hiyo: Antigua na Barbuda, Argentina, Australia, Bahamas, Benin, Bhutan, Bosnia na Herzegovina, Cameroon, Canada, Colombia, Croatia, Jamhuri ya Czech, Jamhuri ya Dominika, Equatorial Guinea, Fiji, Haiti, Hungary, Jamaica, Kiribati, Latvia, Lesotho, Malawi, Mexico, Panama, Paraguay, Ufilipino, Poland, Romania, Rwanda, Visiwa vya Solomon, Sudan Kusini, Trinidad na Tobago, Tuvalu, Uganda, Vanuatu.
Mataifa 128 yaliyounga mkono azimio hilo yalikuwa:
Afghanistan, Albania, Algeria, Andorra, Angola, Armenia, Austria, Azerbaijan
Bahrain, Bangladesh, Barbados, Belarus, Ubelgiji, Belize, Bolivia, Botswana, Brazil, Brunei, Bulgaria, Burkina Faso, Burundi
Cabo Verde, Cambodia, Chad, Chile, China, Comoros, Congo, Costa Rica, Cote D'Ivoire, Cuba, Cyprus
Denmark, Djibouti, Dominica
Ecuador, Misri, Eritrea, Estonia, Ethiopia
Finland, Ufaransa
Gabon, Gambia, Ujerumani, Ghana, Greece, Grenada, Guinea, Guyana
Iceland, India, Indonesia, Iran, Iraq, Ireland, Italia
Japan, Jordan
Kazakhstan, Kuwait, Kyrgyzstan
Laos, Lebanon, Liberia, Libya, Liechtenstein, Lithuania, Luxembourg
Macedonia, Madagascar, Malaysia, Maldives, Mali, Malta, Mauritania, Mauritius, Monaco, Montenegro, Morocco, Mozambique
Namibia, Nepal, Netherlands, New Zealand, Nicaragua, Niger, Nigeria, North Korea, Norway
Oman
Pakistan, Papua New Guinea, Peru, Ureno
Qatar
Urusi
Saint Vincent na Grenadines, Saudi Arabia, Senegal, Serbia, Ushelisheli, Singapore, Slovakia, Slovenia, Somalia, Afrika Kusini, South Korea, Uhispania, Sri Lanka, Sudan, Suriname, Sweden, Uswizi, Syria
Tajikistan, Tanzania, Thailand, Tunisia, Uturuki
Umoja wa Milki za Kiarabu, Uingereza, Uruguay, Uzbekistan
Venezuela, Vietnam
Yemen
Zimbabwe
Mataifa 21 hayakuwakilishwa wakati wa kupigwa kwa kura: Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, El Salvador, Georgia, Guinea-Bissau, Kenya, Mongolia, Myanmar, Jamhuri ya Moldova, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Samoa, San Marino, Sao Tome na Principe, Sierra Leone, Swaziland, Timor-Leste, Tonga, Turkmenistan, Ukraine, Zambia.
www.zakacheka.blogspot.com / www.zakachekainjili.blogspot.com. +255625966236
0 Post a Comment:
Post a Comment