NI KWELI BABA ASKOFU MKUU KAKOBE YUKO KITANZINI?

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>


Nimesoma article kwenye gazeti la Tanzanite iliyoandikwa na mtu anayejiita Odwin Mwandimo yenye kichwa cha habari " Askofu Kakobe kitanzini". Haraka haraka nikadhani amekamatwa na watu wasiojulikana wakamtundika. Nikachukua gazeti, nikatulia nikasoma hiyo article. Nikagundua kumbe huyu Odwin Mwandimo siyo tu ni kanjanja bali pia ni mpuuzi. Article yake has nothing to do with kitundikwa mtu, na wala hakuna mahali po pote ambapo labda Baba Askofu Kakobe alihojiwa akashindwa kujibu hoja. Wakati mwingine katika mazingira haya mtu unaweza kusema amewekwa kitanzini. Lakini huyu kanjanja na mpuuzi anazungumzia mambo anayodai kaambiwa na "waumini" wa Baba Askofu Kakobe ambao hawakutaka majina yao yatajwe. Huyu kanjanja alikuwa anatafuta jinsi ya kuuza gazeti lake la udaku.

Haya ni mawazo yake mwenyewe huyu mpagani asiyemjua Mungu na ndiyo maana hata vifungu alivyovinukuu havina uhusiano wo wote na Baba Askofu Kakobe na mahubiri yake kwa kuwa hajawahi kudharau mamlaka iliyo juu. Kwa mamlaka iliyo juu kuambiwa itubu siyo kuidharau.

Watumishi wa Mungu wameagizwa na Biblia kukemea uovu kwenye jamii hata kama ni mfalme akitenda dhambi pasipo kukusudia atatakiwa kutubu. ( Walawi 4:22-26).

Huyu kanjanja mpagani akazingumzia habari za umeme. Ninakuuliza wewe kanjanja, huo umeme hadi leo unapita? Jibu ni la. Kwa nini? Kwa kuwa Mungu hadhuhakiwi. Wewe Odwin Mwandimo, mpagani na kanjanja, tafuta jinsi nyingine ya kuganga njaa yako.

Kwa taarifa yako, watu wanatakiwa kuwatii wenye mamlaka katika mambo yaliyo mema tu. ( TIto 3:1). Odwin Mwandimo, kama unatafuta kiki, tafuta kwa njia nyingine. Toka hadharani uyataje maneno ya kashfa unayodai Askofu Kakobe alitamka kwa rais Magufuli. Hapa nanukuu andiko lako" Baba  Askofu Kakobe wakati wa siku kuu ya Krismasi mbele ya waumini alitoa maneno mbalimbali yenye kujaa kashfa dhidi ya Serikali na Rais Dk. John Magufuli ndani ya kanisa lake". Mr. Odwin Maandimo, were you there? Watu kama ninyi ndiyo Paulo Mtume aliwakabidhi kwa Shetani ili wafundishwe wasimtukane Mungu. (1Timotheo 1:19-20).

Kwa kusema Askofu Kakobe ana kiburi ambacho wewe unadhani kinasababishwa na kutumika na mashirika ya kijasusi hivyo ni kumtukana Mungu aliyemwita awe mtumishi wake. Kwa nini na wewe Odwin Mwandimo usikabidhiwe kwa Shetani kwa kumtukana Mungu kama akina Himenayo na Iskanda? Kwa nini wewe Odwin Mwandimo Mungu asikulipe sawasawa na matendo yako? (2Timotheo 4:14).

Acha kuwasingizia washirika wa FGBF. Haya ni mawazo yako.

Nami ninamwomba Mungu akulipe sawasawa na uovu wako.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: