Wanafunzi wakiokolewa katika eneo la Tuko.
Watu 17 wameuawa katika mauaji ya watu wengi yaliyofanywa katika shule moja huko Florida Marekani.
Kwa mujibu wa polisi, mtuhumiwa huyo ametajwa kwa jina la Nikolaus Cruz mwenye umri wa miaka 19 na kwamba alikuwa mwanafunzi katika shule hiyo aliyoishambulia.
Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa amebeba bunduki ya kisasa, alianza kushambulia bila ya mpangilio nje ya shule hiyo kabla ya kushambulia ndani, hali ambayo ilisababisha wanafunzi, kuhangaika huku na kule kwa lengo la kujificha chini ya madawati na maeneo mengine.
Kamanda wa polisi katika eneo hilo, amesema mshambuliaji huyo alifukuzwa shule kutokana na utovu wa nidhamu.
Na Tayari polisi walimkamata karibu na mji wa jirani wa Coral Springs.
Shirika la Upelelezila Marekani FBI limesema linashirikiana na polisi, kufanyia uchunguzi tukio hilo.
Shambulio hilo ni kubwa katika siku za hivi karibuni, tangu lile lililoua watu 20, katika shule ya Connecticut 2012.
Katika hatua nyingine, kupitia mtandao wake wa Tweeter, Rais Donald Trump amewaondolea hofu raia, kwa kusema kuwa usalama upo kwa mtoto, mwalimu ama mwingine yoyote yule.
0 Post a Comment:
Post a Comment