Wafuasi wa CHADEMA waliokamatwa msibani jijini Mwanza wapandishwa kizimbani

Wafuasi zaidi ya 10  wa Chadema waliokamatwa wakiwa nyumbani kwa mwanachama mwenzao kuhani msiba wamepandishwa kizimbani.

Watu hao, leo Machi 14, 2018 tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza na kuwekwa katika mahabusu mahakamani hapo kusubiri kukamilika kwa taratibu za kimahakama ili wasomewe mashtaka dhidi yao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi watu hao walikamatwa eneo la Mabatini Machi 13, 20018  baada ya kutokea kutoelewana kati yao na askari polisi.

Amesema askari hao walikuwa wakifuatilia nyendo za wafuasi hao  tangu walipokuwa wakikusanyika kutoka sehemu mbalimbali za Jiji la Mwanza kwenda nyumbani kwa mwanachama mwenzao kwa kile kinachodaiwa ni kuhani msiba.

Katika tukio hilo, polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu zaidi ya 500 waliokuwa kwenye eneo hilo.

Download App YETU hapa⬇⬇



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: