Tanzania ya Viwanda: Viwanda 1,300 vyajengwa ndani ya miezi mitatu

Utekelezaji  wa agizo la ujenzi wa viwanda 100 kwa kila mkoa uliotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, umefikia asilimia 49.4, viwanda 1,285 vikijengwa kati ya 2,600.

Akizungumza katika kikao kazi cha kupitia bajeti ya Tamisemi na mikoa mjini hapa jana, Jafo alisema viwanda hivyo vimejengwa ndani ya miezi mitatu tangu kutolewa kwa agizo hilo.

Alisema agizo hilo bado linaendelea kutekelezwa na kila mkoa unatakiwa kuhakikisha unajenga viwanda 100 kufikia Desemba 31, mwaka huu.

“Viwanda hivi vilivyojengwa vina mchanganyiko mbalimbali vikiwamo viwanda vikubwa, vya kati na vidogo, mna mikakati mikubwa ambayo itawezesha kuwa na mchanganyiko wa viwanda vikubwa na vidogo,” alisema Jafo.

Alibainisha kuwa kupitia wakuu wa mikoa, ajenda ya Rais John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda inatekelezwa na kuwataka waendelee kuitekeleza.


Awali wakuu wa mikoa walitoa taarifa zao za ujenzi wa viwanda hivyo kufuatia agizo alilolitoa huku Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akibainisha kuwa katika mkoa wake tangu kutolewa kwa agizo hilo, viwanda 88 vimeshajengwa.

Hata hivyo, Makonda alisema kumekuwa na changamoto ya umeme na maji na kuiomba serikali kuliangalia suala hilo ili kuendelea kuvutia wawekezaji zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, alisema katika mkoa huo wamejenga viwanda 22 ambavyo ni vikubwa na vya kati na vingine vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

“Changamoto iliyopo ni nishati ya umeme na kwa mkoa wetu tunahitaji tuwe na megawati 800,” alisema Ndikilo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alisema zimetengwa hekari 307,595 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na hadi sasa tangu kutolewa kwa agizo la Jafo, vimejengwa viwanda 45 vipya ambavyo vimetoa ajira mbalimbali.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, alisema mkoa wake unaendelea kutekeleza mkakati wake wa bidhaa moja kwa wilaya moja na kwamba tangu agizo hilo, viwanda 18 vipya vimejengwa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, alisema viwanda vipya vilivyojengwa mkoani kwake ndani ya agizo hilo ni 124 huku Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack, akisema kwake amejenga viwanda 126.


App YETU hapa⬇⬇



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: