Makamu wa rais nchini Cuba, Miguel Díaz-Canel, ametajwa na viongozi wa ngazi za juu nchini humo kuwa ndiye kiongozi mtarajiwa ajaye anayekuja kumrithi ama kuchukua nafasi ya Raul Castro.
Miguel anatajwa kuwa na miaka hamsini na mitano, ambaye kwa taaluma ni mhandisi wa zamani anatarajiwa kuchukua ofisi hii leo, baada ya zoezi la upigaji kura rasmi na mkutano wa kitaifa kuidhinisha uteuzi wake.
Makabidhiano ya madaraka utahitimisha miongo sita ya utawala wa Castro na ndugu yake marehemu Fidel, ambaye aliongoza mapinduzi ya mwaka 1959.
Bwana Diaz-Canel huonekana kama huria kijamii na mbobevu wa teknolojia mpya ingawa hatazamiwi kumaliza mfumo wa chama kimoja nchini humo, ingawa ni mapema mno kumuweka katika nafasi ya namna hiyo kwa sasa.
Raul Castro atasalia kuwa kiongozi mkuu wa Chama cha Kikomunisti mwaka 2021 mpaka mkutano mkuu ujao na anatarajiwa kuendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika jamii yake.
Kwa tabia Miguel ni kiongozi mnyofu na tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa kuwa makamu wa raisi wa baraza la Congress la Cuba mnamo mwaka 2013 ingawa tangu wakati huo amekuwa ni mtu wa karibu wa bwana Castro.
Kwa miaka mitano iliyopita, amekuwa akiandaliwa kushika hatamu za uongozi katika nafasi ya raisi na kupokea madaraka, Ingawa hata kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa makamu wa raisi, amekuwa ni mwanasiasa mkongwe .
Alizaliwa mnamo mwezi wa nne mwaka 1960, mwaka mmoja baada ya Fidel Castro alipokula kiapo cha kushika nafasi ya waziri mkuu.
Miguel Díaz-Canel alisomea masuala ya uhandisi wa umeme na kuanza na kuanza harakati za kisiasa mapema akiwa na miaka 20 kama mwanachama wa chama cha Kikomunisti huko Santa Clara.
Alipokuwa akifundisha uhandisi katika chuo kikuu, Raúl Castro alimsifu kwa "uaminifu wa kiitikadi".
*By Zachary John Bequeker 0758590489*
0 Post a Comment:
Post a Comment