Tundu Lissu apasuliwa tena mguu, amshukuru Mungu kwa kumpigania

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kwa amara nyingine tena, leo Aprili 11, 2018 ataingia kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni ya mguu wake wa kulia ambao bado una matatizo kutokana na risasi alizopigwa Septemba 7 mwaka jana nyumbani kwake, Area D, Dodoma.

Lissu ambaye ameshafanyiwa upasuaji mara kadaa katika Hospitali ya Nairobi nchini kenya kisha Ubelgiji, amesema kwamba oparesheni hiyo ni sehemu ya tiba ya mguu huo huku akieleza kuwa kwenye mikono yuko salama kitabibu. 

"Habari za leo popote mlipo wapendwa wangu. Napenda kuwajulisha kwamba ndani ya nusu saa ijayo ninaingia kwenye operesheni nyingine tena. .

Kama nilivyowataarifu siku za nyuma, mguu wa kulia bado una shida kutokana na risasi nyingi nilizopigwa na 'watu wasiojulikana.' Operesheni ya leo ni sehemu ya tiba ya mguu huo. .

Napenda wote mfahamu kwamba niko kwenye mikono salama ya kitabibu. .

Mungu wetu amekuwa mwema sana kwangu tangu tarehe 7 September ya mwaka jana. Na hili pia litapita. .

Wasalaam."  Ameandika Lissu



Download App YETU hapa⬇⬇





Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: